Habari

Rais Magufuli kupeleka walimu wa Kiswahili Rwanda

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amepokea barua yenye ujumbe kutoka kwa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, iliyowasilishwa kwake na Mjumbe Maalum ambaye ni Waziri wa Elimu wa Rwanda Dkt. Musafiri Papias Malimba.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam, Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze

Rais amepokea barua hiyo, Alhamisi Ikulu, kutoka kwa mjumbe maalum akiwa ni waziri wa Elimu Rwanda Dkt Malimba, aliiwasilisha kwa Rais Magufuli.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa pamoja na kupokea barua hiyo, Mheshimiwa Rais Magufuli na Dkt Malimba wamezungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Rwanda ikiwemo katika sekta ya elimu hususan maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Rwanda kwa kuamua lugha ya Kiswahili ianze kufundishwa katika shule zake na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu wa kwenda kufundisha lugha hiyo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents