Habari

Rais Magufuli: Hakuna mwanafunzi mwenye sifa atakayekosa mkopo

Rais Dk John Pombe Magufuli amewaomba wanafunzi wa elimu ya juu nchini kutulia kusubiri mikopo yao huku akiwahakikishia kuwa hakuna mtu mwenye sifa atakayekosa mkopo.

h1

Rais Magufuli alisema hayo Ijumaa hii wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kusisitiza kuwa pamoja na changamoto hizo hakuna mwanafunzi wa elimu ya juu mwenye sifa atayekosa mkopo huo.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli imekuja wakati ambapo baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu wenye sifa wakiwa katika hali ya sintofahamu baada ya majina yao kutokuwemo kwenye orodha ya kupatiwa mikopo huku wengine wakilalamika kuingiziwa fedha pungufu na hali hiyo kuzua taharuki miongoni mwao.

h10

“Wanafunzi nawaomba mtulie fedha zinatolewa kwa awamu kulingana na utaratibu wenu wa kufungua vyuo hivyo naamini hakuna mtu atakayekosa mkopo kama anastahili kupatiwa na yupo kwenye orodha ya bodi ya mikopo,” alisema Rais Magufuli.

“Lakini naomba niwe very clear (wazi), serikali haitatoa fedha kwa wanafunzi wenye uwezo, nimkute mtoto wa Profesa Rwekaza naye nimpe mkopo? Mtoto wa Profesa Ndalichako na yeye nimpe mkopo? Mtoto wa Kijazi na yeye apate mkopo? Mkopo umelenga kwa ajili ya watoto maskini tu,” alisema.

Aidha rais Magufuli aliwapa onyo bodi ya mikopo kwa kusema kuwa anasikia kuwa katika bodi hiyo kuna upendeleo.

“Nasikia bodi ya mikopo nako kuna upendeleo wa kuwapatia mikopo watu wasiostahili, sitaki siku moja niende bodi nichukue orodha ya wanafunzi wote niangalie shule walizosoma na particular walizojaza halafu nikute majina ya watu wasiostahili kupata mkopo,” alionya.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents