Habari

Rais Magufuli aahidi kuendeleza jitihada za marais waliopita kuwaletea maendeleo wananchi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza jitihada zilizoachwa na Serikali za awamu zilizopita ili kuzidi kuwaletea maendeleo Watanzania.

magu-1

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara yaliyofanyika katika uwanja wa uhuru Jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli alisema ku wa Serikali ya Awamu ya Tano imeanza jitihada za kuboresha huduma za maendeleo ya jamii, ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/17 imeamua kutenga asilimia 40 ya bajeti katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo umeme, miundombinu, afya, elimu.

“Mbali na kujiwekea vipaumbele mbalimbali kwa maendeleo ya nchi, kumekuwa na changamoto kadha wa kadha zinazozikabili nchi ikiwemo ufisadi, rushwa ndani ya baadhi ya watendaji,” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alisema juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali ni kuboresha maslahi kwa watanzania kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuwawajibisha wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli aliwataka watanzania kudumisha amani na kulinda muungano uliyopo kwani amani ni msingi wa maendeleo ya nchi bila amani hakuna maendeleo. Rais Magufuli pia alitoa wito kwa wantanzania kuendelea kufanya kazi kiwa bidii kwani kila mwananchi ana haki ya kufanya kazi, na kusema kuwa waasisi wa nchi walileta uhuru kwa maendeleo ya nchi kwani Uhuru ni kazi.

“Serikali ya Tanzania imejipanga kufanya kazi, tutafanya kazi kwelikweli, watendaji niliowachagua wanafanya kazi hivyo watanzania kwa ujumla mnatakiwa kuonesha ushirikiano kwao kwa maendeleo ya nchi yetu” alisema Rais Magufuli.

Mbali na hayo Rais Magufuli alisema kuwa ndani ya miaka 55 ya Uhuru Tanzania imepata mafanikio makubwa ambapo Tanzania imelinda Uhuru wa nchi, sambamba na kulinda mipaka iliyopo.

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents