Habari

Raia 67 wa Afrika Kusini wafariki kwa kuangukiwa na jengo la kanisa la TB Joshua

Raia 67 wa Afrika Kusini wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na jengo la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua.

TB JOSHUA

Waokoaji wanadai kuwa hostel hiyo ya kanisa ambalo huishi wafuasi wa Nigeria na wa kigeni wa mhubiri huyo, lilianguka kutokana kuzidiwa na ujenzi wa ghorofa zingine. Awali mhubiri huyo alidai kuwa ni watu wachache tu walijeruhiwa na kudai kuwa ndege iliyokuwa ikipaa chini chini ndio iliyosababisha ajali hiyo.

Jumanne alitumia Twitter kuandika; “Hard times may test me, they cannot destroy me.”

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameagiza idara za serikali kusaidia familia za wahanga kwenda Nigeria kutambua miili ya wapendwa wao na kuirejesha nyumbani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents