Habari

Quick Rocka aelezea kwanini ameubadilisha muziki wake ‘sijaacha crunk, najaribu kupiga kwa miguu yote miwili

Hitmaker wa ‘Bullet’ Quick Rocka, amedai baada ya kujikusanyia mashabiki wengi vijana na kuwakonga katika miondoko ya Crunk, trip music na Rap, umefika wakati ameamua kutanua wigo wa mashabiki wa rika tofauti na ndio maana akaamua kufanya aina mbalimbali za muziki.

Quick

“Nimeamua ku-expand fan base yangu ndio maana nikaanza na kufanya “MY BABY” nikaongeza mashabiki wengine watu wazima age fulani wakaanza kunisikiliza na kunielewa,” Quick alikiambioa kipindi cha Bomba Base Show cha Bomba FM Radio ya Mbeya. “Nimetoa hii Penzi ni Rnb slow slow nipo na king wa RnB, Ben Pol ni muziki fulani ambao watu fulani wanaweza pia kunisikiliza,” aliongeza.

“Ila kufanya hivyo haimaanishi kwamba nimeacha kufanya Crunk au trip music niliyofanya miaka minne au mitano iliyopita na watu wakanielewa. Ngoma zipo nyingi siku zinatoka watu watazisikia. Kwahiyo nimejaribu kupiga kwa miguu yote miwili nione kama pande hii pia watu watakubali na vitu kama hivyo lakini so far so good watu wamependa ninavyoimba na ninavyo-rap pia kwahiyo tunasonga pamoja.”

Kusoma “alama za nyakati” ni siri kubwa ya uamuzi wa Quick Rocka kujaribu kufanya muziki wa aina tofauti kutokana changamoto kubwa inayowakabili wasanii wengi kwa kazi zao kutodumu kwa muda mrefu katika chati na kuchuja mapema.

“Kitu kikubwa ni kuonesha uwezo. Unajua nimebarikiwa talent nachana, naimba naweza kubadilika kibiashara, kivyovyote naangalia mimi muziki mzuri nitakaoufanya unakaa muda mrefu sio kwamba mtu atasikiliza miezi miwili halafu anauchoka. Ndio ngoma nyingi ambazo zipo sasa Afro Pop bla bla blaaaaa…. kwaajili ya club watu wameshachoka zinakuja nyingine watu wanaisahau watu wakiipiga wanaforward. Mimi nafanya muziki unaoishi yaani hata baada ya miaka mitatu ukiisikia unasema ‘aaaaa hii ngoma ni kali’, uwe unapenda kusikiliza kama ngoma zile Bullet, 255, My Life ni ngoma nilizozifanya nyuma lakini watu mpaka sasa wanaziappreciate.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents