Burudani

Queen Darleen ahofia kutoa nyimbo mpya kutokana na ushindani kwenye soko la muziki

Vituo vya radio vimekuwa vikipokea kazi mpya za wasanii wa Bongo karibia kila siku, hii ikiwa inamaanisha kuwa ushindani ni mkubwa kutokana na wingi wa wasanii ambao wote wana malengo ya kulikamata soko ambalo wateja wake ni wale wale (mashabiki).

darleen-2
Hali hiyo imekuwa ikiwalazimu wasanii kuwaza nje ya box, ili kuhakikisha kazi wanazotoa hazimezwi na kupotezwa na ushindani huo.

Rapper Queen Darleen amesema kuwa ushindani uliopo kwenye soko la muziki ndio unamsababisha kuchelewa kutoa nyimbo mpya akihofia kutofanya vizuri.

“Unapotoa wimbo kuna ushindani, mwengine atataka kufanya kama wewe unavyofanya, kwa hiyo unampa nafasi yeye je atavuka!?” Alisema kupitia Planet Bongo ya EA Radio.

“mwisho wa siku havuki alafu mi naachi kitu kingine kikali zaidi ya vile alivyovitoa yeye. Mtu anaweza akatoa kazi nne tano na zote zikafeli, lakini mi nikitoa kitu nafanya kwa uhakika na ndio maana natoa audio na video kwa pamoja.” Alisema Darleen.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents