Burudani

Q-Jay kusikika tena kwenye bongo fleva baada ya ukimya mrefu toka aokoke

Baada ya miaka kadhaa tangu mwimbaji wa R&B Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay wa Wakali Kwanza kutangaza kuacha game ya bongo fleva, anatarajiwa kusikika tena kwenye muziki huo katika wimbo mpya.

Q-Jay

Q-Jay ni miongoni mwa wasanii watakaosikika kwenye wimbo mpya wa Dj Aaron unaotarajiwa kutoka Ijumaa (Agosti 29). Dj Aaron amewashirikisha Banana Zorro, Barnaba na Q-Jay katika wimbo huo uitwao ‘Peace One Day’, ambao ni wa kuhamasisha amani.

Miaka kadhaa iliyopita Q-Jay aliyewahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Sifai’, aliamua kuachana na muziki wa kidunia baada ya kuokoka na kutangaza kuwa atakuwa akifanya muziki wa gospel.

Jikumbushie kazi ya Q-Jay ‘Sifai’
http://youtu.be/QcgM8G60mds

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents