Burudani

Q-Chief adai ‘Mkungu wa Ndizi’ inahit kimataifa

Q-Chief amedai amepokea pongezi nyingi kutoka mataifa mbalimbali baada ya wimbo wake aliofanya na TID ‘Mkungu wa Ndizi’ kutoka.

Chilla

Muimbaji huyo amesema ikiwa ni wiki moja tangu aachie wimbo huo, amegundua kuwa umekuwa na mrejesho chanya na mkubwa wa kimataifa kuliko nyimbo zake alizowahi kufanya.

“Mwenyezi Mungu ametenda miujiza,” ameiambia Bongo5. “Sina jibu kwa nini wimbo wangu unanya vizuri zaidi nje, hata mimi nashangaa simu za nje ni nyingi sana kuhusu huu wimbo. Nimepigiwa siku nikaambiwa wimbo unachezwa Nigeria, hii ni hatua kubwa sana katika muziki wangu na ni wimbo wangu wa kwanza kufanya vizuri kwa muda mchache,” ameongeza.

“Mimi naendelea kuzishukuru media pamoja na mashabiki wote ambao wamenipokea kwa mikono miwili.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents