Burudani

Q Chief adai bado ana nafasi ya kuwa mshindani kwa wasanii wanaofanya vizuri sasa

Msanii wa muziki aliyewahi kuwika katika kipindi cha nyuma na wimbo ‘Si Ulinikataa’ na nyingine, Abubakar Katwila ‘Q Chief’ amefunguka kwa kusema kuwa bado yupo katika mapambano ya kuhakikisha anarudi kwenye chati na kushindana na wasanii ambao wanafanya vizuri kwa sasa.

Muimbaji huyo ambaye yupo mbioni kusafiri kwenda Afrika Kusini kwajili ya kushoot video ya wimbo wake ‘Koku’ aliomshirikisha Patoranking, ameiambia Bongo5 kuwa bado anaona kuna mambo makubwa yanakuja ambayo yatawashangaza mashabiki wake wa muziki.

“Mungu bado yupo pamoja na mimi mpaka sasa, mengi nimepitia lakini sasa hivi nipo vyema kabisa, kwahiyo suala la ushindani kwenye muziki linaamriwa na kazi nzuri, na muziki mzuri,” alisema Q Chief. “Mimi binafsi sioni ugumu wa kusema nisifanye vizuri zaidi ya fulani, ukongwe wangu unasaidia sana kwa sababu nimepitia vingi kwa hiyo najua nini natakiwa kufanya,”

Muimbaji huyo amedai bado anaendelea kujiweka sawa katika muziki wake huku akiwataka mashabiki wa muziki wake kusubiria surprise kubwa kutoka katika muziki wake.

Q Chief kwa sasa anafanya kazi chini ya label QS Mhonda Entertainment.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents