Burudani

Promota wa show ya Diamond iliyosababisha fujo Ujerumani adai wawekezaji walimzunguka

Kampuni ya Britts Events iliyokuwa imeandaa show ya Diamond mjini Stuttgart, Ujerumani imetoa maelezo ya chanzo cha kutofanyika kwa show hiyo na pia kuzuka kwa fujo iliyosababisha uharibifu mkubwa kwenye ukumbi uliokuwa utumike.

Britts
Mwenyekiti Mtendaji wa Britts Events, Awin Williams Akpomiemie

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Awin Williams Akpomiemie ameeleza kwa kina katika maelezo ambayo Bongo5 tumeyatafsiri kwa Kiswahili hapo chini.

Watu wangu awali ya yote, ningependa kuelezea moyo wangu kwa kuuambia umma na mashabiki wa Diamond Platnumz, kwamba sisi kutoka uongozi wa Britts Events tunaomba radhi kwa kile kilichotokea usiku uliopita, wakati wa show ya Diamond Platnumz. Haikuwa imepangwa show ichelewe kuanza au kwa msanii kutotumbuiza. Hapa ntawaeleza ukweli wote wa kile kilichotokea katika tamasha hilo kwakuwa ninyi nyote mnataka kuujua ukweli.

Mradi wa Diamond ulikuwa wa gharama kubwa sana kwakuwa uongozi Britts Events ulitaka kila kitu kiwe professional. Kama kampuni tuliamua kutafuta wawekezaji watakaowekeza kwenye mradi huu hivyo tuliwafuata wawekezaji watatu lakini mmoja wao hakuwekeza sana kwani alidai hatokuwa nchini.

Wawekezaji wawili ni watu wanaofahamika sana jijini Stuttgart, mmoja anafanya kazi na jeshi la Marekani na mwingine anamiliki kampuni ya usafirishaji mjini Stuttgart. Hawa ndio wawekezaji wakubwa tuliowapata. Tuliwapa mikataba wasaini lakini yule mwenye kampuni ya usafirishaji alikataa kusaini mkataba wa mradi huo kwakuwa alitaka kuwa na mkataba wake binafsi na yule jamaa wa Marekani. Kisha nilimwambia Mr.USA kuwa hiyo haikuwa hatua sahihi lakini Mr.USA alisema ‘Britts msiwe na shaka, kila kitu kitakuwa poa.

wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg

Watu wangu, mradi ulianza na kisha wale wawekezaji wawili wakagundua kuwa Diamond ni msanii mkubwa na angevuta umati mkubwa wa watu na watu wanampenda. Kisha walijiunga pamoja dhidi ya Britts waliowaalika kama wawekezaji kwenye mradi huo na walitaka kuuchukua kutoka kwa Britts sababu ni wao ndio walioleta sehemu ya fedha kwaajili ya mradi huu wakati Britts ndio wanaommiliki msanii na mradi wenyewe. Ila tu kwakuwa Britts ni kampuni mpya mjini Stuttgart, Mr. Shipping Guy aliamua kuungana na yule jamaa wa Marekani na DJ Wanted, kuuchukua mradi.

Pindi Britts ilipokaa chini na kufanya mkutano nao, walikuwa wakifanya mkutano wao wenyewe na kubadilisha mipango yote hivyo walikuwa wanahujumu na kuendelea na mradi nyuma ya Britts. Britts ina makubaliano nao kuwa pindi msanii atakapowasili Ujerumani, watampa balance ya 3.250 euros, na walikubaliana na kigezo hicho kwasababu Diamond aliweka wazi kuwa bila fedha asingepanda ndege.

Waliniomba mimi niongee na Diamond kuwa watampa fedha kwenye uwanja wa ndege, lakini unajua nini? Kabla Diamond hajawasili Mr. USA na Mr. Shipping Guy pamoja na DJ Wanted walitaka kuandaa wahuni kumuiba msanii kutoka kwenye show ya Britts lakini Britts walikuwa wajanja na walimchukua msanii kabla hawajafanya chochote. Hapo ndipo shida ilipoanzia.

Huko Essen kabla Britts haijafika huko, USA Guy na Shipping Guy, walikuwa wameshapeleka wafanyakazi wapya kuchukua show na kuwafuza wafanyakazi wa mwanzo. Kisha Britts ilikuwa ikilumbana nao kuwa wao ni wawekezaji tu na sio waratibu wa kampuni, kwanini wanataka kuhodhi tukio kwasababu mnataka kutengeneza fedha na sio kujali watu. Britts baadaye ilikuja kugundua kuwa wafanyakazi waliowapeleka walikuwa wapenzi wao wa zamani na ndugu zao.

Dhumuni la kufanya hivyo lilikuwa ni kuiba fedha na kutofuata mkataba na Britts, hivyo baada ya Diamond kuwasili Stuttgart usiku wa saa tano, alikuwa amechoka lakini wawekezaji hawakujali. Walikuwa wakifirikia tu jinsi wanavyoweza kurudisha fedha zao. Diamond alisema anahitaji fedha yake lakini Shipping Guy na USA Guy walikataa kumpa fedha Diamond wakihisi kuwa Britts wanataka fedha ya ziada.

Kisha usiku ulipoingia sana, waliweza kutoa 3.000 euros na ilikuwa saa tisa na nusu tayari lakini Diamond aliendelea kukataa kutumbuiza kwakuwa alidai ni lazima wamlipe fedha iliyosalia ambayo ni 250 euros, kitu ambacho ni haki yake kutokana na makubaliano.

Mpaka muda Mr Shipping Guy na Mr USA Guy wanagundua kuwa Britts walikuwa wakifanya kitu sahihi kwa kuwaomba walipe fedha hizo kwa Diamond, tulikuwa tumeshachelewa na watu walikuwa wameshaanza kupigana wakati huo Diamond alikuwa ndani ya gari mbele tu ya ukumbi, na kama ningemruhusu atoke wangemuua.

Tunavyoongea hapa, Mr USA anadai kuwa fedha tulizoingiza kwenye tukio zima ziliibwa na watu hivyo Britts Events haiwezi kupata fedha kutoka kwenye tukio tuliloliandaa na kulimiliki. Hiyo ilikuwa mipango yao kuchukua biashara ya mtu mwingine kutokana na tamaa.

Britts Events inawapenda, Britts Events ilitaka kila mtu awe na furaha, Britts Event haijawahi kuahidi msanii yeyote na asije. Na niamini hata tulipofanya show ya Bracket tulikuwa na kitu kile kile kutoka kwa wawekezaji. Walipoona kuwa show inaweza kuwa na mafanikio walitaka kupewa asilimia 50% ya kampuni.

Well, sitakiwi kusema yote haya kwakuwa ni jambo la uongozi lakini niliamua kuweka mambo sawa, siwezi kuficha tena. Tuna Waafrika wengi wenye tamaa wanaotaka kuchukua biashara za watu wengine sababu ya tamaa. Lengo letu ni kuwafanya muwe na furaha na sio kupoteza muda na fedha zenu. Tunafahamu kuwa nyote mlitoka sehemu za mbali, mliacha watoto wenu na familia.

Uongozi wa Britts Events unaomba radhi kwa hili. Hivyo msiilamu Britts Events lakini laumuni tamaa za Mr. USA Guy na Mr. Shipping Guy. Tunawapenda na tunaahidi show ya bure ya Diamond hivi karibuni.

Maelezo yake kwa Kiingereza ni hayo chini:

MY PEOPLE FIRST OF ALL, I WOULD LIKE TO EXPRESS MY HEART BY TELLING THE GENERAL PUBLIC AND THE FANS OF DIAMOND PLATNUMZ, THAT WE FROM BRITTS EVENTS MANAGEMENT IS VERY SORRY FOR WHAT HAPPENED LAST NIGHT, DURING THE CONCERT OF DIAMOND PLATNUMZ. IT WAS NEVER PLANNED FOR THE CONCERT TO BE DELAYED OR FOR THE ARTIST NOT TO PERFORM.
HERE I WOULD TELL YOU ALL THE TRUTH OF WHAT REALLY HAPPENED ABOUT THIS EVENT FOR YOU ALL TO KNOW THE TRUTH.
THE PROJECT OF DIAMOND CONCERT WAS A VERY EXPENSIVE PROJECT.

BECAUSE THE BRITTS EVENTS MANAGEMENT WANTED EVERYTHING TO BE PROFESSIONAL, AS A COMPANY WE DECIDED TO LOOK OUT FOR INVESTORS WHO WOULD INVEST IN THIS PROJECT, THEN WE APPROACHED THREE INVESTORS WHO INVESTED BUT ONE OF THEM DID’NT INVEST TOO MUCH AS HE SAID HE WONT BE IN THE COUNTRY.

THE TWO INVESTORS ARE WELL KNOWN PEOPLE LIVING IN STUTTGART
ONE WORK WITH THE USA MILITARY THE SECOND ONE OWNS A SHIPPING COMPANY IN STUTTGART, THESE WERE THE TWO MAJOR INVESTORS THAT WE GOT, WE GAVE THEM A CONTRACT TO SIGN AND ONE OF THEM SIGNED BUT THE SHIPPING GUY REFUSE TO SIGN THE CONTRACT OF THE PROJECT THAT HE WANTS TO HAVE A PRIVATE CONTRACT WITH THE USA GUY, THEN I TOLD MR.USA THAT WAS A WRONG MOVE BUT MR.USA SAID BRITTS DO NOT WORRY,ALL WILL BE FINE,

MY PEOPLE THE PROJECT STARTED AND THEN THE TWO INVESTORS THEN NOTICE THAT DIAMOND IS A BIG ARTIST AND HE WOULD PULL LOTS OF CROWD AND PEOPLE LOVE HIM, THEN THEY TEAMED UP AGAINST BRITTS WHO INVITED THEM AS INVESTORS ON THIS CONCERT AND WANTED TO TAKE THE PROJECT AWAY FROM BRITTS BECAUSE THEY ARE THE ONE WHO BRINGS PART OF THE MONEY FOR THIS PROJECT WHILE BRITTS IS THE ONE WHO OWNS THE ARTIST AND THE PROJECT,.

JUST BECAUSE BRITTS IS A NEW COMPANY IN STUTTGART MR. SHIPPING GUY DECIDED TO TEAM UP WITH THE USA GUY AND DJ -WANTED, TO TAKE OVER THE PROJECT, WHEN BRITTS SITS DOWN AND HOLD MEETINGS WITH THEM, THEY WOULD DO THEIR OWN MEETING AND THEN,CHANGE ALL THE PLANS BEHIND BRITTS MANAGEMENT, SO THEY WERE OPPRESSING AND PUSHING THE PROJECT BEHIND BRITTS.

BRITTS HAVE AGREEMENT WITH THEM THAT WHEN THE ARTIST ARRIVE GERMANY THEY WOULD GIVE HIM THE BLANCE OF 3.250 EUROS, AND THEY AGREED TO THIS TERM BECAUSE DIAMOND MADE IT CLEAR THAT WITHOUT THE MONEY HE WOULD NOT FLY, THEY ASKED ME TO TALK TO DIAMOND THAT THEY WOULD GIVE HIM THE MONEY RIGHT AT THE AIRPORT, BUT DO YOU KNOW WHAT? BEFORE DIAMOND ARRIVED, MR.USA AND MR.SHIPPING GUY TOGETHER WITH DJ WANTED, ARRANGED FOR THUGS TO STEAL THE ARTIST FROM BRITTS EVENTS BUT BRITTS WAS SMARTER AND TOOK AWAY THE ARTIST BEFORE THEY COULD MAKE ANY MOVE, THAT WAS WHERE THE TROUBLE STARTED FROM, IN ESSEN BEFORE BRITTS ARRIVED THERE, USA GUY AND SHIPPING GUY ,ALREADY BRING IN NEW WORKERS AND
SECURITY TO TAKE OVER THE SHOW, AND DROVE AWAY THE ORIGINAL WORKERS .

THEN BRITTS WAS FIGHTING WITH THEM THAT THEY ARE JUST INVESTORS AND NOT THE COMPANY MANAGER, WHY DO YOU WANT TO STEAL THE EVENT BECAUSE YOU WANT TO MAKE MONEY AND NOT CARING ABOUT THE PEOPLE, BRITTS THEN NOTICE THAT THE WORKERS THEY BROUGHT WERE THEIR EX-GIRL FRIENDS AND RELATIVES.

10649568_792593844095765_1264697582686012878_n

THE REASON WHY THEY DID THIS WAS TO STEAL THE MONEY AND NOT TO FOLLOW THE CONTRACT WITH BRITTS, SO WHEN DIAMOND ARRIVED STUTTGART LATE NIGHT AT 11.PM, HE WAS NOT TOO FINE BUT THE TWO INVESTORS DO NOT CARE.

THEY WERE ONLY THINKING ABOUT HOW THEY WOULD GET THEIR MONEY BACK,DIAMOND SAID HE NEEDS HIS MONEY BUT SHIPPING GUY REFUSE USA GUY TO GIVE DIAMOND THE MONEY , THINKING THAT BRITTS EVENTS WANTS EXTRA MONEY .

THEN WHEN IT WAS ALREADY TOO LATE THEY MANAGED TO BRING OUT 3.000 EUROS THEN IT WAS 3.30AM ALREADY , BUT DIAMOND REFUSED TO STILL PERFORM BECAUSE HE SAID THEY MUST GIVE HIM HIS BLANCE OF 250 EUROS , WHICH IS RIGHT CAUSE THAT WAS THE AGREEMENT.

BY THE TIME MR SHIPPING GUY AND MR USA GUY REALISED THAT BRITTS WAS DOING THE RIGHT THING BY ASKING THEM TO PAY UP THE MONEY TO DIAMOND IT WAS ALREADY TOO LATE CAUSE PEOPLE HAVE STARTED FIGHTING,WHILE DIAMOND WAS RIGHT INSIDE THE CAR IN FRONT OF THE VENUE,IF I LET HIM OUT THEY WOULD KILL HIM, AS WE ARE TALKING RIGHT NOW, MR. USA SAID THE MONEY WE MADE FROM THE WHOLE EVENT WAS STOLEN BY THE PEOPLE, SO BRITTS EVENTS CAN’T GET MONEY FROM THE EVENT WE ORGANISED AND OWNED .

THESE WHERE THEIR PLANS TO TAKE OVER ANOTHER MANS BUSINESS DUE TO GREED.

BRITTS EVENTS LOVE YOU GUYS, BRITTS EVENTS WANTED EVERYONE TO BE HAPPY, BRITTS EVENT HAVE NEVER PROMISED ANY ARTIST AND THE ARTIST DID’NT COME,.

AND TRUST ME WHEN WE DID BRACKET EVENT WE HAD THE SAME EXPERIENCE THE SAME THING FROM THE INVESTORS , AS SOON AS THEY SEE THAT THE EVENT WOULD BE A SUCCESS THEY STARTED ASKING FOR 50% OF THE COMPANY.

WELL AM NOT SUPPOSE TO SAY ALL THESE HERE AS ITS A MANAGEMENT ISSUE,BUT I DECIDED TO CLEAR THE AIR I CAN’T KEEP IT ANY MORE , WE HAVE LOTS OF GREEDY AFRICANS OUT THERE WHO WANTS TO TAKE AWAY PEOPLES BUSINESS JUST BECAUSE OF GREED.

OUR AIM IS TO MAKE YOU ALL HAPPY, NOT TO WASTE YOUR TIME AND MONEY , WE KNOW THAT YOU ALL CAME FROM FAR PLACES, LEFT YOUR KIDS AND FAMILY . BRITTS EVENTS MANAGEMENT IS REALLY VERY SORRY ABOUT THIS.

SO DO NOT BLAME THIS ON BRITTS EVENTS BUT BLAME IT ON THE GREED OF MR USA GUY AND MR. SHIPPING GUY. WE LOVE YOU AND WE PROMISE YOU A FREE SHOW EVENT WITH DIAMOND VERY SOON…. JUST LOOK OUT.
Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook
You might also like:

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents