Burudani

Professor Jay kufuata nyayo za Mpoto na Jide katika kusambaza album yake mpya atakayotoa 2014

Licha tatizo la usambazaji wa album bongo lililowafanya wasanii wengi kusitisha kutoa albums kwa kuhofia kupata hasara, rapper Joseph haule aka Professor Jay ameahidi kutoa album mpya mwaka huu (2014), ambayo itakuwa ni album yake ya tano.

JAY

Rapper huyo mkongwe ambaye hivi karibuni ametoa single mpya iitwayo ‘Kipi sijasikia’, amesema ana mpango wa kutumia njia walizotumia Lady Jaydee na Mrisho Mpoto katika kusambaza album zao zilizopita, kusambaza album yake mpya itakayoitwa ‘Izack mangesho’.

“Kweli sasa hivi kwa wadosi pale kunasumbua…lakini tuna mpango wa kuongea pia na Max Malipo”, amesema Professor Jay kupitia Magic Fm. “Unajua Max Malipo wapo karibu kila sehemu kwahiyo wanaweza kusambaza kazi zetu. Kama Mrisho Mpoto alianza kuuza album yake kwa style hiyo..hata dada Jaydee pia naona aliiuza mwenyewe kwa style hiyo..so na mimi nadhani naweza kupitia njia hiyo lakini kwa kuiboresha zaidi”.

Album za Professor Jay zilizopita ni ‘Machozi Jasho na Damu- 2001’, ‘Mapinduzi Halisi -2003’, ‘J.O.S.E.P.H- 2006’, na ‘Aluta Continua -2007’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents