Burudani

Hammer, Cigar, Bakora, Casino: Professor J ni mdosi kwenye video ya Tatu Chafu (Picha)

Safari hii Joseph Haule aka Professor Jay ni kama ameamua kulipa deni alilonalo kwa mashabiki wake, sababu amesema hataki kuweka gap la ukimya tena, itakuwa ni mwendo wa bandika bandua.

Jay2

Baada ya kutoa single ya ‘Kipi Sijasikia’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz mwezi April, hivi karibuni ameachia audio ya single nyingine inayoitwa ‘Tatu Chafu’.

Licha ya kuwa video ya ‘Kipi Sijasikia’ aliyoshoot na Adam Juma wa Visual Lab: Next Level mwezi uliopita (July) bado haijatoka, tayari ameanza kushoot video ya single mpya ‘Tatu Chafu’ chini ya mwongozaji Hefemi.

Jay3

Kupitia Instagram Jay ameshare picha za BTS ya utengenezaji wa video ya ‘Tatu Chafu’

“Day one. .. Madirector na maproducer wetu tukiwawezesha WANAWEZA , Asante Mungu. .. #Hatuachii Gap #Nakung’ata mchana kweupeee kama MBU wa DENGU #puna Nikupune #BACK2BACK MUZIK #STRICKLY HIPHOP #TheMastermind of the GAME #Nilimshawishi baba yako akuruhusu Uimbe. ..UNABISHA??? @hefemi @nkwabi1 @adamjumanxl @nisherbybee @majani187 @marcochalitz @fresh120media” Aliandika Professor Jay

Jay1

“#TATUCHAFU video. …#MGodi unaotembea kwenye HIP HOP GAME #puna nikupune #Hatuachi gap tena mpaka waombe POOH #MWANALIZOMBE #Video directed by @hefemi Three Locations to GO. #God is great!!! “Aliandika

Jay5

“Day one…. #TATUCHAFU Video in the making. .. ASANTE MUNGU kwako hakuna kinachoshindikana.. . Two locations down , Three to go!!! Work work work”. Aliandika kwenye moja ya picha.

Jay4

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents