Habari

Professor Jay aongea hiki baada ya mbunge wa Kilombero kuhukumiwa kwenda jela miezi 6

By  | 

Baada ya mbunge wa Jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali na Dereva wake, John Kibasa kuhukumiwa kwenda jela miezi sita bila faini kwa kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi mwaka 2015, Professor Jay ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi ameumizwa na kitendo hicho.

Kupitia ukurasa wa facebook wa Professor ameandika:

Wanadhani wanatutisha ili tuogope Na kurudi nyuma, Hawajui kuwa WANATUKOMAZA Na kutuongezea Ujasiri zaidi wa Kuendeleza Mapambano. Ipo Siku TUTAELEWANA TU na Jela tutaona kama tumekwenda DISCO! Congratulations Mpiganaji @mh.lijualikali Hatujui kesho ni zamu ya nani ila WE ARE VERY READY!! TRUST ME. ALUTA CONTINUA.

Mbunge huyo wa Kilombero atatumikia adhabu ya miezi 6 jela na baada ya kumaliza hukumu hiyo na kuachiwa huru ataendelea na kazi yake ya ubunge kama kawaida kwani sheria inasema mbunge akifungwa jela zaidi ya miezi sita kwa kosa lolote basi atapoteza nafasi yake ya ubunge.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments