Burudani

Professor J auzungumzia wimbo ‘Kwaajili Yako’ f/ Chameleone unaotoka J5 hii

Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Joseph Haule aka Professor Jay Jumatano hii anaachia ngoma yake mpya aliyomshirikisha Jose Chameleone.

10844224_776874095719292_2068212298_n

Proffesor amesema wimbo huo unazungumzia mapenzi pamoja na kutoa shukrani kwa mashabiki wanao-support muziki wao.

“Tumeanza kushirikiana kuanzia kwenye idea mpaka unarekodiwa kwenye studio yangu ya Mwanalizombe,” ameiambia Bongo5. “Idea kwenye hii Kwaajili Yako imefika time inabidi tu- give back kwenye society. Pia unahusu mapenzi ni kwajili ya mpenzi wako, lakini pia ni kwaajili ya mashabiki. Professor Jay na Chameleone ni wasanii nguli ni wasanii ambao tumekuwa pamoja kwa muda mrefu sasa tukaona hii pia iwe kama asante kwa kumaliza mwaka 2014 kwa mashabiki wetu. Ni wimbo ambao unaweza ukawa na maana mbili kwa mtu umpendae, shabiki, anaweza akawa demu ndio maana tukaita kwaajili yako au Just for you na vitu kama hivyo,” alisema Professor.

Kuhusu video ya wimbo huo Professor amesema: Video inakuja lakini kwakuwa Chameleone ameniomba niende Uganda niende kum-support kwenye show yake One kwahiyo tunafikiria kui-shoot huko huko kipindi ambacho nitaenda kwenye hiyo concept inayofanyika kesho kutwa. Lakini kuna uwezekano mkubwa tukashoot huko huko lakini kuna uwezekano mkubwa tulikuwa tumepanga either tushoot Uganda au South Africa.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents