Burudani

Professor J ajishirikisha mwenyewe kwenye ‘Tatu Chafu’ kwa majina ya J Hussle na Nigga J

Rapper mkongwe Professor J anatarajia kuachia single yake mpya iitwayo ‘Tatu Chafu’ iliyotayarishwa kwenye studio yake ya Mwanalizombe chini ya producer Villy.

Profesa J alikuwepo kuwaipa support timu ya  Adam Juma

Akiongea na Bongo5 leo, Professor amesema kwenye wimbo amewashirikisha J Hussle na Nigga J ambao hata huvyo ni yeye mwenyewe.

“Watu walikuwa wana kiu sana na mimi siku nyingi nilikuwa sijarelease ngoma kwahiyo nikaona sio haki kuendelea kuwaweka juujuu kwa sababu wanakosa chakula cha ubongo ambao na kirelease,” amesema J. “Watu wengine walikuwa wakilalamika sana wengine wakidhani uwezo wangu umepungua so nataka kuprove kuwa ‘am the best in East Africa’ na sehemu nyingine zote, ukiongeza ghuba ya Uaajemi nakadhalika,” ametamba rapper huyo.

“Pia kitu kikubwa ni kwamba nitoe shukrani kwa mashabiki wamenipokea vizuri na nimedumu kwenye game kwa muda mrefu na sasa hivi ni kipindi cha sikukuu za Ramadhan watu wanastahili kuwapa vitu vizuri zaidi. Kwahiyo kuanzia sasa hivi siwezi kukaa muda mrefu bila kurelease ngoma kwa sababu ushindani kusema ukweli umekuwa mkubwa na malengo yetu ya kwenda international yapo pale pale. Hatuwezi kukaa kimya muda mrefu wakati wenzetu wanatoa ngoma mara kwa mara zenye ubora ili waende zaidi kimataifa. Siongelei soko la bongo tu naongelea soko la kimataifa ambalo sasa hivi kila mtu analikodolea macho,” ameongeza.

“Hii ngoma inayofuata nimeifanya kwenye studio yangu ya Mwanalizombe chini ya producer Villy lakini video pia nafanya na Hefemi na video tunaanza kushoot kesho kila kitu kipo stand by. Kwahiyo itakuwa ni nafasi ndogo sana kati ya ‘Kipi Sijasikia’ narelease na hii ngoma. Video zinaweza zikatoka zote kwa pamoja lakini audio inaweza ikatoka soon kuna vitu vidogo vidogo tunavimalizia lakini kila kitu kipo tayari. Wimbo Tatu Chafu nimefanya kama Professor Jay ft. J Hussle na Nigga J lakini wimbo wote nimeimba mimi. Sema J Hussle ni yule wa zamani ambaye alikuwa na uimbaji fulani na Nigga J huyu ni wa kipindi cha katikati na ndani ya wimbo huo huo kuna Professor huyu wa sasa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents