Burudani

Profesa Jay: Siwezi tena kuimba Singeli

Rapper mkongwe Profesa Jay amefunguka kuwa hatoimba tena muziki wa Singeli.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumatano hii, Jay amesema, “Mimi napenda kusapoti vipaji vilivyopo mitaani, hata leo ukinipa jezi nicheze mpira ili kuhamasisha watu waupende mpira nitacheza lakini siyo sehemu yangu.”

“Kuhusu Singeli mimi siwezi tena kuimba nilivyoimba ule wimbo nilitaka kuonesha jamii kuwa kuna muziki huu pia upeni ushirikiano. Sasa wasanii wenye wimbo huo ndiyo wenye jukumu la kuhakikisha unakua lakini mwaka huu wameonekana kupooza wanatakiwa wapambane,” ameongeza.

Kwa sasa rapper huyo ameachia wimbo wake mpya ‘Kibabe’ ambao umeanza kufanya vizuri japo una siku moja tangu alipouachia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents