Burudani

Profesa Jay kuachia ngoma aliyomshirikisha Dully Sykes


Baada ya Kamiligado, the heavyweight MC nchini Tanzania, Joseph Haule anatarajia kuachia ngoma yake mpya muda sio mrefu.
Wimbo huo uitwao Hellow amemshirikisha Dully Sykes aka Mr. Misifa.
Jana kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema:
“Greetings. I have got great news. I am about to release my new track titled “HELLOW” featuring DULLY SYKES .You wanna be the first to hear it? Send me your e-mail address and STAY TUNED…LEGOO!!”
Mpaka sasa Profesa Jay ambaye anasifika kwa kuwa miongoni wa wasanii wa kwanza kwanza nchini kuupa heshima muziki wa kizazi kipya, tayari ana ameshatoa albam nne tangu aanze muziki ambazo ni pamoja na Machozi Jasho na Damu, 2001, Mapinduzi Halisi, 2003, J.O.S.E.P.H 2006 na Aluta Continua 2007.
Miongoni mwa tuzo alizowahi kushinda ni pamoja na, albam bora ya hip hop 2004 (“Mapinduzi Halisi”) , wimbo bora 2006, (Nikusaidiaje), mwandishi bora wa nyimbo 2009 zote za Kili Music Awards, wimbo bora wa kitanzania 2006 ya Kisima Music Awards ,na zingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents