Burudani

Profesa Jay asikitishwa na wasanii wa Bongo Flava waliopotezea mazishi Mzee Gurumo

Msanii mkongwe wa Hip Hop, Profesa Jay ameeleza kusikitishwa kwake kutokana na wasanii wengi wa muziki ya Bongo Flava kushindwa kwenda kumzika msanii mkongwe wa muziki wa dansi Muhidin Gurumo aliyefariki Jumapili iliyopita na kudai kuwa wasanii wengi waliishia kuandika tu R.I.P.

1509771_10152345930292558_5133216687622541981_n
Profesa Jay akiwa kwenye mazishi ya Mzee Gurumo Jumanne hii katika kijiji cha Masaki, Kisarawe mkoani Pwani

Profesa Jay amesema hayo wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Capital FM.

“Kiukweli ilinisikitisha sana kwasababu wasanii kule Kisarawe kiukweli tulikuwa wachache sana,” alisema. “Sikumwona mwingine sijui hatukuwa karibu karibu, kwasababu labda watu walikuwa wengi lakini kiukweli niliona wengi wazee ambao nilikutana na akina Abdul Salvado tukasalimiana, akina Mze Mabela kutasalimiana, akina Ali Choki ndio niliwaona kule na vitu vingine kama hivyo. Lakini wasanii wa kizazi kipya kiukweli hawakuonyesha hivyo vitu. Lakini nimeona wanapost wanasema, Rest in peace mzee, Rest in peace mzee, lakini physically hawakuonyesha ushirikiano,iliniumiza kidogo nikasema tupo mjini hapahapa ofcourse wengine wamebanwa wako nje ya mkoa,walikuwa mbali au wengine majukumu yaliwabana, lakini sio kiasi hicho tupo wengi sana. Tungeweza kuonyesha hivi vitu ni lazima tutokee kwa mfano. Inasikitisha kidogo labda watu waliona uvivu kuona Kisarawe mbali,lakini Kisarawe ni hapa tu,” alisema Profesa Jay.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents