Profesa Jay akanusha kumtapeli promota wa Mombasa, asema yeye ndiye anadai!!

JIZEE

Hivi karibuni gazeti la The Star a nchini Kenya liliandika kuwa rapper Joseph Haule aliingia kwenye mgogoro mkubwa na promoter wa mjini Mombasa Kenya aliyemchukua kufanya show na kumshutumu kuwa amemtapeli.

Prof alikuwa amechukuliwa kufanya show mbili siku ya Christmas kwenye kumbi za Jamboree Resort na Quetu Beach Resort.
Hata hivyo kwa mujibu wa website ya mtangazaji wa East Africa Radio, Sam Misago, Profesa amethibitisha kuwa taarifa hizo si za kweli.

Website hiyo imeandika kuwa Jay alikubaliana na promoter huyo aitwaye Eljah Ngirimani wa kampuni ya Black Slate ya mjini Mombasa kuhusu show 2 ambazo zilikuwa tarehe 24 December iliyofanyika Jambori na Tarehe 25 Iliyofanyika Kwetu Beach. Show zote Prof Jay alizifanya kama ilivyopangwa ila ulipofika muda wa kulipwa ndio matatizo yalianza.

Amesema promoter huyo alishindwa kumlipa pesa alizotakiwa kumlipa na kwa sasa bado promoter huyo anadaiwa na Prof Jay shilingi 120,000 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 2 za Tanzania.Amedai kila akipigiwa simu promoter huyo alikuwa akimwahidi Jay kumlipa baadae lakini hakufanya hivyo.

Mchawi huyo wa rhymes amesema promoter huyo hakulipa hata nauli yake ya kurudi Tanzania na Ilibidi ajilipie nauli mwenyewe na watu wake na ndio maana aliondoka kabla ya kufanya show ya tarehe 31 December mjini Mombasa.Jay amesema ameshtushwa na taarifa hizi kwani yeye ndiye anadai na sio kudaiwa chochote na anaamini promoter huyo ameamua kuongea uongo kwenye vyombo vya habari ili kulinda jina lake.

Promoter huyo aliliiambia gazeti la The Star kuwa Profesa Jay hakuwa amelipwa fedha zote kwa show ya pili na hivyo alipewa camera aina ya Nikon D3000 kama rehani.Baada ya show, Prof aliondoka nchini Kenya na crew yake na kuibeba kamera hiyo.

Issue hiyo imekuwa kubwa kiasi ambacho passport ya mpambe aliyekuwa amesafiri na Jay nchini humo imeshikiliwa ili asiondoke.Waandaaji wanadai kuwa walimlipa Profesa Jay shilingi 252,000 za Kenya ambazo ni zaidi hata ya fedha walizokuwa wamekubaliana na sasa wanataka warudishiwe fedha yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents