Burudani

Pop it in: Alikiba na Jokate wathibitisha uhusiano wao kwa picha hizi!

Fresh Jumbe aliwahi kusema penzi ni kikohozi kulificha huwezi.

11325466_1438202943152520_1548326419_n

Na sasa penzi la Jokate Mwegelo na Alikiba limefikia hatua ambayo haliwezi kuwa siri tena. Wawili hao wamekuwa wakidaiwa kuwa wapenzi kwa miezi kadhaa sasa lakini bado binafsi hawajeza kukubali wala kukataa.

Lakini sasa huenda hatua za awali za kuelekea kuuweka hadharani uhusiano huo zimeanza kufanyika. Alianza Jokate aliyepost selfie kwenye Instagram akiwa na msanii huyo aliyejipa jina la King Kiba na kutoandika chochote. Picha hiyo imepata likes 13,215 na comments 824.

Naye Kiba jana alipost selfie nyingi kwenye akaunti yake ya Instagram na kuandika: Pop It In @jokatemwegelo #KingKiba.” Picha hiyo imevutia likes 8108 na comments 680.

11374694_105245623144751_1882656243_n

Huenda picha hizo zikawa ni tangazo rasmi la uhusiano wao. Kuna tatizo moja lakini – Jokate aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents