Habari

Polisi akutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Daudi Mwangosi

Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani askari Polisi, Pacificius Cleophace Simoni, kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mwanahabari Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
mwangosi-2

Kwa mara ya kwanza Simoni alifikishwa mahakamani hapo Septemba 12 mwaka 2012 akituhumiwa kufanya kwa kukusudia mauaji hayo wakati mwandishi huyo alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari kwenye ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri umeilazimisha mahakama hiyo chini ya Jaji Kihwelo kuibadili kesi hiyo kutoka kwenye mauaji ya kukusudia na kuwa mauaji ya bila kukusudia ambayo hukumu yake ameisogeza mbele hadi kesho Jumatano.

Baada ya mabadiliko hayo, wakili wa upande wa Jamhuri, Adolph Maganga, aliiomba mahakama hiyo imhukumu mtuhumiwa huyo kifungo cha maisha jela kwa mujibu wa Kifungu cha 198 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu huku wakili wa utetezi, Lwezaula Kaijage akiiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu kwa kumfunga kifungo cha nje.

Source: Habari Leo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents