Burudani

PNC adai anayumba kimuziki kutokana na kukosa uongozi, atangaza kutafuta management ya kumsimamia

Msanii wa muziki PCN ambae hapo mwanzo alikuwa chini Mtanashati Entertaiment, ametangaza kutafuta management ambayo itakuwa inasimamia kazi zake za muziki.

PNC

Akizungumza na bongo5 leo, PNC amesema msanii bila usimamizi hawezi kwenda kokote kutokana na muundo wa muziki ulivyo.

“Muziki wetu sasa hivi unaitaji mambo mengi sana licha ya kuandika na kuimba,nataka mtu au kampuni ambayo ina uwezo wa kumsimamia msanii, unaujua muziki ukoje, ambayo itanifanya nikapiga hatua kubwa, siyo magumashi magumashi. Unajua wasanii wengi tunayumba kutokana na kukosa uongozi mzuri, kwa sababu mimi naamini naweza kufanya kazi nzuri, natakiwa kupata uongozi ambao utaweza kusimamia kazi zangu nikaweza kupiga hatua kubwa zaidi kama watu wengine walivyoweza kupiga hatua , napata changamoto nyingi sana mimi siwezi kuusimamia muziki wangu wote nikaweza, kuna kazi nyingi sana, msanii anatakiwa kushauriwa yani vitu vingi sana” Amesema PNC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents