Burudani

Pipi azungumzia changamoto ya kufanya muziki akiwa ndani ya ndoa

Msanii wa muziki na mama wa watoto wawili, Pipi Doreen, amefunguka na kuzungumzia changamoto ya kufanya muziki huku akiwa ndani ya ndoa.
PIPI

Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo ‘Hafai’, ameiambia Bongo5 kuwa ndoa yake haimletei matatizo katika muziki wake.

“Mimi naona hakuna tatizo kufanya muziki nikiwa ndani ya ndoa,” alisema Pipi. “Sema wakati nikienda kazini nawakumbuka sana watoto wangu, nakumbuka sana nyumbani na familia yangu,”

Aliongeza, “Hakuna kinachoingilia kazi yangu kwa sababu mtu ambaye amenioa ni mtu ambaye nilikuwa naye kabla sijaanza muziki,”

Pia muimbaji huyo amewataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi nyingi zaidi ambao aliziandaa akiwa analea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents