Burudani
Pina kuizindua albamu
Mkari kutoka katika Kikosi cha Mizinga aka 41 ,Karapina anatarajia kufanya ‘Bonge’ la onyesho la Hip hop litalokusanya wanaharakati wa Hip hop toka Afrika Mashariki, katika uzinduzi wa albamu yake ya Nyimbo Tosha yenye nyimbo zaidi ya Ishilini.
Alisema katika tamasha hilo, litalo fanyika usiku wa tarehe 27, mwezi wa huu atafanya kumbukumbu wa sanii wa Hip Hop kama Niga O,Raf Nelly, Bilob, Cone Frances. ilikuwaezi kutokana na mchangao wao mkubwa katika muziki huo.
Aliongezea kwa kusema pia kutakuwa na matamasha ya Karate, mavazi na Free style Battle na wasanii wa Afrika mashariki wakiwa Ay, Mwana Fa, Godzilla, Madee,Mansoor na BoB toka Tanzania, wakati Rwanda atakuja Back T, na Kenya atakuwepo Kimya na Ukoo Fulani.