Picha/Video: Huddah Monroe akiwasili JK Nyerere International Airport – Dar
Dar es Salaam mko tayari kwa Huddah Monroe? Mrembo na mwakilishi huyo wa Kenya kwenye shindano la Big Brother Africa 2013 aka The Chase amewasili jijini Dar es Salaam leo asubuhi akitokea jijini Nairobi Kenya tayari kwa kuhost party kubwa ya katikati ya mwaka, Mid Year Bash itakayofanyika kesho Jumamosi pande za Elements.
Huddah akiwa na mwenyeji wake, Arthur wa kampuni ya Unity Entertainment kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam
Mid Year Bash imeandaliwa na kampuni ya SK Entertainment kwa kushirikiana na Unity Entertainment huku wadhamini wakiwa ni pamoja na Heineken, Vodacom na Bongo5. Kiingilio ni shilingi 20,000 tu.
Huddah baada ya kuwasili
Arthur na Huddah wakielekea kwenye gari
Huddah akiwaupdate mashabiki wake wa Twitter baada ya kuwasili Dar
Huddan na Arthur wakielekea kwenye gari kwenda hotelini