Burudani

Picha: Zari amfuata Diamond Nigeria?

Licha ya kuwa Diamond Platnumz hakuongozana na mpenzi wake Zari The Boss Lady kwenda Nigeria Jumatatu hii, lakini kuna uwezekano mkubwa wawili hao wakawa pamoja kwenye hafla ya ugawaji tuzo za michezo za Glo-CAF Awards itakayofanyika Alhamisi Jan 8 jijini Lagos, ambapo Platnumz ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza.

Zari

Zari The Boss Lady amepost picha (hapo juu) asubuhi ya leo Jumatano (Jan 7) akiwa kwenye ndege na kuandika “Another day, another flight. Stay blessed”, inayoashiria kuna uwezekano mkubwa akawa anaenda kwa baby wake Nigeria.

Diamond Lagos

Diamond naye jana alipost picha zake mwenyewe (hapo juu) akiwa anaonekana mpweke na kuandika, “Kuna mtu alikuwa mnyooonge na mpweke jana…” hii inamaanisha mtu muhimu ambaye ni baby wake ndiye anayekosekana.

Baada ya kuwa pamoja Uganda kwenye party ya Zari mwishoni mwa mwaka jana, Zari na Diamond walisafiri pamoja kwenda Burundi na Rwanda na ndio sababu kuna kila dalili pia watakua pamoja Nigeria licha ya kuwa hawakusafiri pamoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents