Michezo
Tazama picha za uwanja mpya wa Chelsea utakaokamilika 2020
Huu ndio muonekano wa uwanja mpya wa klabu ya Chelsea ya Uingereza ambapo hadi mwaka 2020 ujenzi utakuwa umekamilika.
Kwa sasa klabu hiyo bado ipo kwenye mazungumzo na wakazi wa maeneo utakapojengwa uwanja huo. Mmiliki Chelsea, Roman Abramovich ana mpango wa kutumia pound milioni 500 katika ujenzi wa uwanja huo ili pia uwe na biashara tofauti inayojitegemea mbali na Chelsea.
Ujenzi huo unatarajiwa kuanza baada ya miezi 9 kuanzia hivi sasa na klabu ya Chelsea itabidi kuhama uwanja wao wa Stamford Bridge na kutumia Uwanja wa Wembley kwa kipindi cha misimu mitatu.
Uwanja huo mpya wa Stamford Bridge utakuwa unachukua mashabiki 60,000 ambao ni sawa na uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam. Uwanja wa sasa wa Chelsea unachukua watu wasiozidi 41,000.