Burudani

Picha za Diamond na Zari the Boss Lady zilizowashtua wengi ni ‘video shoot’ ya wimbo

Mfanyabiashara na mwimbaji mrembo wa Uganda, Zari the Boss Lady na Diamond Platnumz waliingia kwenye headlines weekend iliyopita baada ya picha zao wakiwa kwenye faragha kama wapenzi kuzua maswali mengi kwenye mitandao ya kijamii.

dz

Hata Hivyo Zari hakuchukua muda mrefu na kuamua kutumia Instagram kufumbua fumbo hilo kwa kuweka wazi kuwa ameshirikiana na Diamond katika wimbo wake mpya.

Zari ameuambia mtandao wa Big Eye wa Uganda kuwa picha zilizosambaa ni sehemu ya video shoot ya wimbo aliofanya na hit maker wa Number 1.

dz2

Wimbo huo unatarajiwa kutoka December 18 wakati wa party ya Zari ‘All white Ciroc party’ itakayofanyika kwenye Club Guvnor nchini Uganda.

Kitu ambacho watu wengi walikuwa hawafahamu ni kuwa , Zari ni muimbaji lakini alikuwa ameweka pembeni muziki kwa muda, na sasa ameamua kurejea.

Tazama video ya moja ya nyimbo alizowahi kutoa

http://youtu.be/S9b4_KU2GQU


Source: Big Eye

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents