Burudani

Picha: Wema Sepetu na Penny wamaliza tofauti zao, wakumbatiana na kupiga picha pamoja

Hatimaye mpenzi wa sasa (Wema) na mpenzi wa zamani (Penny) wa msanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz wamemaliza tofauti zao zilizotokana na ‘penzi’ la hit maker huyo wa ‘Number 1’.

Penny n Wema2
Penny, Junaithar aliyewapatanisha, na Wema

Muigizaji wa Bongo Movie Wema Sepetu na mtangazaji wa E-FM Penny Mungilwa a.k.a VJ Penny walikutana usiku wa jana kwenye birthday dinner ya rafiki yao aitwaye Junaithar ambaye ndiye aliyewapatanisha.

Penny n Wema3

Picha za Wema na Penny wakikumbatiana huku nyuso zao zikiwa na tabasamu zimeashiria kuwa sasa kila mmoja ameacha yaliyopita na hana kinyongo na mwenzake.

Penny n Wema
Penny na Wema wakifurahi

Kupitia Instagram Junaithar aliyewapatanisha aliandika:

“Wema na penny leo wamemaliza tofauti zao nilijuwa wema kupitaa penny nawapenda sana wadogo zangu @wemasepetu_auntyezekiel @vjpenny04 @nsepetu”

Picha: Instagram

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents