Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Picha: Wema Sepetu aachiwa kwa dhamana, Manji na Gwajima watinga polisi

By  | 

Alhamisi hii malkia wa filamu nchini Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni tano baada ya kupandishwa kizimbani kwenye mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka matatu yanayomkabili.

Wakati huo huo mfanyabiashara maarufu Yusuph Manji na askofu Josephat Gwajima wamewasili katika kituo cha kati cha polisi kwa ajili ya kutii agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paulo Makonda ambapo majina yao yalitajwa Jumatano hii kuwa miongoni mwa majina 65 katika orodha ya watu wanatuhumiwa kuhusika na madawa ya kulevya.

Tazama picha zaidi hapa chini.

Petit Man akimuongoza Wema kupanda gari baada ya kuachiwa kwa dhamana

Mwanasheria Albert Msando akiteta jambo na Wema ambaye yupo ndani ya gari

Mama Wema akiwa katika eneo la mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi ya mwanae

Wafuasi wa Gwajima wakiwasili kituo cha kati cha polisi Dar es Salaam

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW