Habari

Picha: Washindi wa The Mabati Cornell Kiswahili Prize for African Literature wakabidhiwa zawadi

Washindi wa tuzo za The Mabati Cornell Kiswahili Prize for African Literature wamekabidhiwa tuzo zao pamoja na zawadi ambazo waliahidiwa.

Idrissa Haji Abdalla akikabidhiwa tuzo na Mama Salma Kikwete

Washindi wawili usiku huo walijiondokea dola 5000 huku mmoja akiondoka na dola 3000.

Shughuli hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam mgeni rasmi alikuwa Mama Salma Kikwete pamoja Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura.

Pia waandishi wakongwe wa vitabu pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali walihudhuria.

Usiku huo burudani ilitolewa na msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto akishirikiana na B Band ya Banana Zoro.

Washindi.

Fiction
1. Idrissa Haji Abdalla (Tanzania), for Kilio cha Mwanamke ($5,000)
2. Hussein Wamaywa (Tanzania), for Moyo Wangu Unaungua ($3,000)

Poetry
1. Ahmed Hussein Ahmed (Kenya), for Haile Ngoma ya Wana ($5,000)

Picha za matukio mbalimbali.


Ahmed Hussein Ahmed (Kenya) akikabidhiwa tuzo na Mama Salma Kikwete

Hussein Wamaywa (Tanzania)

Mrisho Mpoto akiteta jambo na Mama Salma Kikwete


Mrisho Mpoto/Banana akiwa pamoja na mwandishi wa kitabu cha Mabala the Farmer, Richard Mabala


Meneja wa B Band, Banana Zoro akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents