Habari

Picha: Wanasayansi wagundua sayari mpya inayofanana na dunia

Wanasayansi wamegundua sayari inayokaribiana sana na dunia kwa mazingira na ukubwa ambayo inaizunguka nyota ya Proxima Centauri inayokaribiana zaidi na mfumo wetu wa jua.

Proxima 1

Sayari hiyo imepewa jina la Proxima b, inapatikana umbali wa kilomita trilioni 40 na kwa kutumia teknolojia ya sasa ya vyombo vya usafiri wa anga za juu inaweza ikachukuwa maelfu ya miaka kuifikia sayari hiyo ambayo inaizunguka nyota ya Proxima Centauri inayozunguka katika eneo ambalo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupatikana kwa maji.

“Kusema kweli, kufika huko kwa sasa hiyo ni kama hadithi ya kubuni kisayansi, lakini watu sasa wanalifikiria hilo na si jambo lisiloweza kufikirika kwamba wakati mmoja huenda watu wakatuma chombo huko,” amesema Guillem Anglada-Escudé ni mtafiti ambaye kundi lake la Pale Red Dot limechapisha matokeo ya ugunduzi wa sayari hiyo katika jarida la Nature.

Proxima 3

Mapema mwaka huu, bilionea Yuri Milner alisema atawekeza $100m katika utafiti wa kuunda chombo au kifaa kidogo kinachoweza kusafiri anga za juu kwa kutumia teknolojia ya laser ambacho kitarahisisha safari ya kuifikia sayari hiyo kwa 20 ya kasi ya mwanga kutoka maelfu ya miaka hadi miongo kadha.

Takwimu kutoka kwenye darubini ya HARPS iliyowekwa nchini Chile inaonyesha uzito wa Proxima b huenda ukawa mara 1.3 zaidi ya uzito wa dunia na kwamba inazunguka nyota ya Proxima katika umbali wa kilomita milioni 7.5 na huchukua siku 11.2 kumaliza mzunguko mmoja.

Proxima 2

Umbali kutoka kwenye nyota ya Proxima Centauri hadi kufikia sayari hiyo ni mfupi ukilinganisha na umbali kutoka kwa dunia hadi kwa Jua ambapo umbali wake ni kilomita 149 milioni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents