Habari

Picha: Wakazi wa Kibamba wauzuia msafara wa Makonda wakidai kudhulumiwa ardhi

Wakazi wa Kibamba Wilayani Ubungo wamezuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonesha kuwa wamedhulumiwa ardhi yao.

Msafara wa Makonda ukiwa umesimama baada ya wananchi kuziba njia kutaka fidia zao

Mapema leo mchana mkuu huyo wa mkoa alitembelea mradi wa chuo cha tiba shirikishi cha Muhimbili kilichopo Kibamba ndipo wananchi hao walipoziba geti lakutokea kwenye chuo hicho huku wakiwa na mabango yanayoonyesha madai ya kudhulumiwa ndipo Mkuu wa wilaya ya Ubongo Humphrey Polepole alipoamua kushuka na kuzungumza  na wananchi hao.

Akiongea na wakazi hao mkuu huyo amewataka wakazi hao kufuata utaratibu kwani madai yao yamefika mezani kwake na baadhi yamenza kushughulikiwa kwa watu kulipwa fidia zao kutokana na kupisha eneo la chuo na hospitali ya MUHAS .
DC Polepole amesisitiza kuwa serikali ipo pamoja na wAjax hao ambao wengine wanadai fidia ya eneo la kwembe na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alihaidi kuwa watalipwa, vilevile Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alihaidi kuwa serikali itazifanyia kazi ahadi zote zilizoachwa na serikali iliyopita.

DC Polepole ameongeza kuwa kwa wale wakazi waliopo maeneo ya hifadhi ya barabara serikali itaendelea na msimamo wake wa upanuzi wa barabara kama alivyohaidi Rais Magufuli jana kwenye Mkutano wa hadhara wa RC Makonda uliofanyika Maramba Mawili.

Kwa upande wake RC Makonda ambaye alishuka baada ya wakazi hao kuonekana kugoma kupisha msafara huo nakuwaambia kufuata utaratibu kutokana na majibu ya awali ya DC Polepole.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents