Picha

Picha: Vodacom Tanzania yazindua mtandao wa 4G wenye kasi zaidi

Kampuni ya Vodacom Tanzania Alhamis hii ilizindua rasmi mtandao wa 4G utakaowawesha wateja wake wa jijini Dar es Salaam kupata internet yenye kasi zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akizungumza kwenye uzinduzi huo

Uzinduzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza kwenye uzinduzi huo

Akiongea kwenye uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alisema kuwa spidi ya mtandao wa 4G wa Vodacom haina tofauti na ile inayopatikana kwenye nchi zilizoendelea.

Alisema kuwa mtandao huo utatumika kama chachu ya maendeleo kwenye sekta nyingi nchini.

“4G kwetu sio teknolojia, 4G kwetu ni kiwezeshaji, ni kiwezeshaji kwa serikali, kiwezeshaji kwa biashara, ni kiwezeshaji kwa watumiaji wetu,” alisema. “Inachofanya inafungua fursa mpya, uwezekano mpya,” aliongeza.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao

Ferrao alisisitiza kuwa wapenzi wa burudani nchini watafurahia Zaidi kutoka na spidi yenye kasi ya mtandao huo ambayo hawajahi kuishuhudia. “HD Streaming, upakuaji wa muziki wenye kasi ya ajabu, hakuna tena maudhi ya kusubiri, inakuwezesha kuwa na uunganishwaji wa muda wote.”

Alisema mtandao wa 4G utarahisisha masuala muhimu kama mikutano inayofanyika kutumia mawasiliano ya video, ufanyaji masoko kwa njia ya kidijitali.

Muimbaji wa kundi la Mafikizolo,  Nhlanhla Nciza akitumbuiza mbele ya watu mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Mlimani City
Muimbaji wa kundi la Mafikizolo, Nhlanhla Nciza akitumbuiza mbele ya watu mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo kwenye ukumbi wa Mlimani City

Kwa upande wake Rosalynn Mworia ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, amewataka wateja wa Vodacom kwenda kwenye maduka yao ili kuweza kubadilishiwa laini zao za simu na kupewa mpya zilizowezeshwa na teknolojia ya 4G.

Wafanyakazi wa Vodacom wakiwaunganisha wateja waliohudhuria uzinduzi huo na mtandao wa 4G
Wafanyakazi wa Vodacom wakiwaunganisha wateja waliohudhuria uzinduzi huo na mtandao wa 4G

“Kwa kifupi ni kwamba mteja ataweza kupata internet ambayo ina spidi kuliko zote na ataweza kudownload kama ni movie akaziangalia live bila buffering,” alisema.

Mshereheshaji, Taji Liundi akimhoji mteja wa Vodacom kuhusu kasi ya internet anayoipata baada ya kuanganishwa na 4G
Mshereheshaji, Taji Liundi akimhoji mteja wa Vodacom kuhusu kasi ya internet anayoipata baada ya kuanganishwa na 4G

Bi Mworia aliongeza kuwa pamoja na mteja wa Vodacom kupata laini ya 4G, bado atapewa vifurushi vya bure vya internet zikiwemo GB 4 atakazoweza kuzitumia ndani ya masaa 48. “Lakini pia kwa mwaka mzima, kila anaweka vocha na kujiunga na kifurushi, anapata GB 1 ya nyongeza ambayo ina validity ya mwaka mzima

Mameneja wa Diamond, Salam na Babutale wakiwa na mwandishi wa Bongo5, Rama Nnauye
Mameneja wa Diamond, Salam na Babutale wakiwa na mwandishi wa Bongo5, Rama Nnauye

Wageni waalikwa wakishuhudia show ya Mafikizolo
Wageni waalikwa wakishuhudia show ya Mafikizolo

Wanamuziki wa kundi la Mafikizolo wakitumbuiza
Wanamuziki wa kundi la Mafikizolo wakitumbuiza

IMG_6213

IMG_6230

IMG_6236

IMG_6251

IMG_6275

IMG_6276

IMG_6277

IMG_6283

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents