Picha: Vanessa Mdee na Nancy Sumari waiunga mkono kampeni inayowataka wasichana kujitambua
Asasi ya wanafunzi wa kike waliojitolea na kuchukua hatua ya kuwaelimisha wasichana wenzao kwa kuwafundisha haki zao, TEEN GIRLS SUPPORTIVE INITIATIVE jana imeendelea na kampeni inayohamasisha wasichana kujitambua kwa kupinga mimba za utotoni.
Wasichana hao ni Lydia Chales,Janeth Edward na Scholastica Wilson jana walikuwa katika shule ya sekondari Jamhuri jijini Dar es Salaam na kuungana na wanawake wenye mafanikio katika nyanja tofauti wakiwemo Nancy Sumari, Emelda,Vanessa Mdee,Jokate Mwegelo na Joyce Kiria ambao waliwahamasisha wasichana walio kwenye shule hiyo kutambua haki zao na wajibu wao katika jamii.
Wasichana wa asasi hiyo walipata nafasi ya kujifunza sheria zinazowatetea kutoka TAWLA “TANZANIA WOMEN LAWYERS” na wakaamua kuanzisha TEEN GIRL SUPPORTIVE INITIATIVE ili kuwaelimisha wenzao juu ya haki zao na fursa wanazostahili kuzipata na pia kuendelea kuwahamasisha wasichana wote. Kauli mbiu yao inasema “Msichana jitambue uwe chachu ya maendeleo”.