Habari

Picha: Ujenzi wa Hotel ya kwanza Afrika Mashariki kujengwa kwenye maji ndani ya ziwa Victoria wasimama

Mwaka 2013 ujenzi wa hotel ya kwanza Afrika Mashariki itakayokuwa katikati ya maji kwenye ziwa Victoria ulianza nchini Uganda, huku ukigharamiwa na serikali ya nchi hiyo.

Mgahawa unaoelea
Mchoro wa jengo la hotel hiyo

Hotel hiyo inayotarajiwa kuwa na ghorofa nne, moja ikiwa ni ya mghahawa, ya pili ikiwa na vyumba vya kulala na mbili zinazosalia ni kwaajili ya matumizi mengine ilitarajiwa kukamilika baada ya miaka miwili toka ujenzi uanze.

Mgahawa unaoelea-2
Hatua za awali za ujenzi wa hotel hiyo, picha ya mwaka 2013

Taarifa za sasa zinasema kuwa ujenzi huo umesimama kutokana na ukosefu wa shilingi bilioni 2 za Uganda (zaidi ya 1,252,000,000 TSH) zinazohitajika kuweza kukamilisha ujenzi huo.

Source: Daily Monitor

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents