Habari

Picha: Sitti Mtemvu akanusha kuwa na mtoto, asema ana miaka 23, hatovuliwa taji

Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amevilaumu vyombo vya habari kwa kueneza habari za uongo kuhusiana umri na maisha yake binafsi. Mtemvu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Miss Tanzania Sitti
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumanne, October 21

“Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho hapo kinajielezea, mkitaka mnaweza kwenda hizo sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti. Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha kuzaliwa kilipotea akidai kuwa ni kutokana na maisha yake ya kusafiri mara kwa mara.

IMG_6541
Sitti Mtemvu na mama yake wakiondoka baada ya kukutana na waandishi wa habari

“Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,” alijitetea.

“Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo,” alijibu mrembo huyo baada ya waandishi wa habari kumtaka awape ripoti yoyote ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha mwanzo.

Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.

IMG_6522
Hashim Lundega akionesha cheti cha kuzaliwa cha Sitti Mtemvu

Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,” alisema.

Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1989 na huku kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa May 31, 1991, Sitti alisema:

Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’ niliombwa cheti cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life, kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja anachukua passport yetu, ama driving licence ya kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni kitu ambacho mngependelea.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim Lundenga alisema kuwa nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na umri na maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo watavifanyia kazi.

IMG_6524
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited Hashim Lundenga akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni Miss Tanzania, Sitti Mtemvu

“Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana na mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua taji, vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema Lundenga.

Kuhusu Sitti kudanganya kuwa na umri wa miaka 18 kama watu walivyodai ndivyo alivyosema, Lundega alidai kuwa hayo yamezushwa mtandaoni na kwenye shindano hilo hakuna aliyesema hivyo.

“Unaamini kwamba Sitti ana miaka 18?” alihoji Lundenga. “Sasa kama huamini yote yametoka kwenye vyombo vya habari. Sisi tunaamini cheti cha kuzaliwa, sasa kama kuna mtu ana doubt na cheti cha kuzaliwa aende RITA akafanye uchunguzi wake.”

Wasikilize hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents