Habari

Picha: Sheria Ngowi amvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu wakati wa kuapishwa

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa kutoka Tanzania, Sheria Ngowi amepata nafasi ya kumvalisha suti maalum (Presidential suit) Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kuwa Rais mpya wa nchi hiyo zilizofanyika Jumapili (Jan 25) katika viwanja vya ‘National Heroes’ mjini Lusaka-Zambia.

Rais wa Zambia-1
Rais Edgar Lungu (kulia) akiwa amevaa suti iliyobuniwa na Sheria Ngowi

Ngowi ameelezea jinsi alivyoweza kupata nafasi hiyo alipozungumza na Power Breakfast ya Clouds Fm leo.

“Ilitokea tu by chance nikapata chance ya kukutana na mheshimiwa akapenda kazi yangu, basi baada ya hapo akaniambia nataka univalishe napoapishwa nikishinda, nikamwambia nashukuru sana nitafanya hivyo. Basi mi nilichukulia mzaha lakini ikaja kuwa ni kitu kiko serious. Basi wiki moja kabla matokeo hayajatoka nikapigiwa simu kwamba nahitajika kwaajili ya kumfanyia vipimo, basi nikaondoka nikaenda kumfanyia vipimo, nilifika kule ( Zambia) basi ndo nikawa ni mmoja kati ya watu walikuwepo kushuhudia siku anaapiishwa Rais mpya ambayo ilikuwa Jumapili , basi baada ya hapo imekuwa tena historia nyingine tena kwangu.”Alisema Ngowi.

Ngowi Zambia
Sheria Ngowi akiwa kwenye sherehe hizo Lusaka-Zambia, “With My Zambian Family from my right Dada Sophia Nyerere and Mr.Emmanuel Mwapa at Inauguration ceremony of President of the Republic of Zambia HE Edgar Lungu in Lusaka Today.” aliandika kwenye picha hiyo

Rais wa Zambia-3

Sheria ameongeza kuwa haikuishia kumvalisha Rais huyo wakati wa tukio la kuapishwa tu bali yeye ndiye atakuwa anamvalisha kila wakati kwenye matukio tofauti.

“Nitakuwa namtengenezea nguo zake za design tofauti kwa kifupi namvalisha” alisema Ngowi.

Rais wa Zambia-4

Rais wa Zambia-2

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents