Burudani

Picha: Serengeti Fiesta yagawa dozi ya burudani Bukoba

Baada ya tamasha la Serengeti Fiesta linalodhaminiwa na kinywaji mashuhuri cha Premium Serengeti kutoa burudani murua jijini Mwanza wiki iliyopita, imepeleka burudani ya aina ileile katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.

08
Ommy Dimpoz akitumbuiza kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba

Ikidumisha kasumba yake ya kutoa burudani halisi kwa wapenzi wake, Premium Serengeti iliwapeleka wasanii mashuhuri kutoka pande zote nchini. Ilipofika majira ya saa kumi jioni, uwanja wa Kaitaba ulikuwa umefurika mashabiki kutoka pande mbalimbali wakisaka tiketi za kuingilia ukumbini.

01
Msanii wa kundi kijulikanacho kama International, Moses Nyama akiwaongoza wenzake wakati wa onyesho la
Serengeti fiesta 2014, lililofanyika jana jioni Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba

“Umati ulikuwa mkubwa sana…tiketi ziliisha mapema na ikatuladhimu kutafuta njia za kupata tiketi nyingine ili kila mwana Bukoba aliyefika uwanjani apate fursa ya kushuhudia burudani ya kweli,” alisema Meneja wa bia ya Serengeti, Rugambo Rodney.

10
Meneja wa Bia ya Serengeti, Rugambo Rodney (kulia) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mama Zipora Pangani wakati wa tamasha la Serengeti fiesta katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba

02
Ommy Dimpoz’,akiwapa mkono baadhi ya mashabiki wake katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana jioni

Uwanja wa Kaitaba ulizizima kwa shangwe pale mototo wa nyumbani, Saida Kalori alipopanda jukwaani huku akiporomosha burudani ya asili.

03
Msanii maarufu wa nyimbo za asili, Saida Karoli, akilitawala jukwaa wakati wa onyesho la Serengeti Fiesta

07
Nay wa Mitego

Shabiki wake waliozidi 15,000 waliruka kwa shangwe huku wakicheza nyimbo asilia kama vile Chambua kama karanga,maria salome, kaisiki, mapenzi kizunguzungu na nyingine nyingi. Wasanii wengine waliokamata jukwaa ni pamoja na Ommy Dimpoz, Young Killa, Barnaba, Madee, Jux, Ney wa Mitego, Stamina, Blue, Linah, Christian Bella, BK Sande, Luteni Kalama na Mo Music.

04
Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi. Khamis Kagasheki (kulia), akimpongeza mmoja wa wasanii walioshinda katika Mashindo yaliyojulikana kama dansi la Serengeti fiesta 2014, Joylen Hamis, wakati wa tamasha la Serengeti fiesta kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba

Kwa mujibu wa Serengeti, kundi hili la wasanii lililotoa burudani Bukoba ndilo lItakalokwenda kushusha mvua ya burudani huko Kahama siku ya Jumapili. Tamaha la burudani la fiesta Bukoba liliambatana pia na shindano la kuimba lililowashirikisha wasichana wadogo lijulikanalo kama Serengeti SupaNyota Divas.

05
Barnaba Boy akitumbuiza kwenye uwanja wa Kaitaba

Mshindi aliyepatikana Bukoba ataambatana na washidi wengine jijini Dare es Salaam ili kumpata mshindi wa mashindano hayo mwaka huu. Baada ya Mwanza, Bukoba tamansha hili litaelekea mjini Kahama, na baada ya kahama, burudani hili la nguvu litashuka mikoa mbalimbali kama Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Tanga, Moshi, Arusha, Mtwara na Dar es salaam na hatimaye jijini Dar es Salaam ifikapo oktoba 18 mwaka huu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents