Burudani
Picha: Samantha (Hotshots) abariki kava la single ya msanii wa Tanzania
Aliyekuwa mwakilishi wa Afrika Kusini kwenye shindano la Big Brother Africa 2014, Samantha anaendelea kufurahia maisha nchini alikokuja kumpa kampani Idris Sultan.
Pamoja na kutoweka wazi, wawili hao wanahisiwa kuwa ni wapenzi. Mrembo huyo ameamua kulibariki kava la wimbo mpya wa Milian, Until Forever Ends utakaotoka hivi karibuni.
“Until forever ends album cover @milliandollarboy. Download link coming soon, love the song.Thank you and Congrats,” ameandika Samantha.