Burudani

Picha: Ommy Dimpoz aipeleka ‘Tupogo’ VOA Swahili/English

Ommy Dimpoz hana ‘phobia’ ya lugha ya Kiingereza na ndio maana hakuukacha mwaliko wa idhaa ya Kiingereza ya Sauti ya Amerika aka VOA kwaajili ya interview leo.

IMG-20130920-WA002
Ommy Dimpoz akiwa kwenye studio za VOA idhaa ya Kiingereza

Hitmaker huyo ambaye yupo nchini Marekani kwa ziara ya wiki tatu ambapo kesho ataperform jijini Washington DC, alizitembelea studio hizo zilizopo kwenye mji huo mkuu wa Marekani kuzungumzia masuala mengi kuhusu muziki wake.

IMG-20130920-WA003
Ommy Dimpoz akihojiwa na mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America, Sunday Shomari

“Wamenihoji kuhusu muziki nilipoanza, matatizo ya wasanii kutumia madawa, kuelezea tour yangu, malengo ya baadaye na mengine,” Ommy ameiambia Bongo5.

IMG-20130920-WA005

“Nimejifunza vya kutosha kwamba hili ni shirika kubwa sana, wana idhaa 42,” aliongeza.

IMG-20130920-WA001

IMG-20130920-WA000

Kuhusu show yake ya kesho mjini Washington, Ommy amesema: Nimejiandaa vya kutosha, watu wanasubiri kwa hamu hususan Watanzania na Wakenya. Meza za VIP ni sold out tayari, wengine watakata tiketi kwenye show, kiingilio ni dola 30 kawaida.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents