Burudani
Picha: Mwana FA, Jokate, Nick wa Pili na wasanii wengine wampa ‘tick’ January Makamba
Kuna kila dalili kuwa kizazi kipya kinahitaji kiongozi anayekielewa vyema.
January Makamba amewashaweka wazi nia yake ya kuingia kwenye mchakato wa kuwania uongozi wa juu wan chi – urais na tayari kundi kubwa la mastaa wa Tanzania limeonekana kumpa shavu.
Hivi karibuni wasanii kadhaa wameonekana wakipost picha zao wakiwa wameshika kitabu ‘Maswali 40/Majibu 40: Mazungumzo na January Makamba’ na huku wakinukuu baadhi ya mambo aliyosema mbunge huyo wa Bumbuli na naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Miongoni mwa mastaa hao ni pamoja na Mwana FA, Lamar, Nick wa Pili, Shilole, Jokate, Barnaba, Babu Tale, Yamoto Band, Peter Msechu na wengine.