Habari

Picha: Mtoto afariki baada ya wazazi kujaribu kumsukumia oxygen kwa mikono, kutokana na hospitali kukosa umeme baada ya kimbunga kuikumba Philippines

Mtoto mwenye umri wa siku tatu amejikuta akipoteza maisha baada ya wazazi wake kujaribu kadri ya uwezo wao kuokoa maisha yake kwa kutumia kifaa cha kuingiza hewa mdomoni kwa mikono, badala ya mashine kutokana na hospitali kukosa umeme baada ya maafa ya kimbunga yaliyoikumba Philippines hivi karibuni.

Mtoto Philippine1
Mama akijaribu kumsukumia oksijen kwa mkono mwanae

Baba na mama wa mtoto huyo walilazimika kupeana zamu ya usiku na mchana kwa siku hizo tatu ya kusukuma hewa kwa kutumia kifaa kidogo (kama chupa ya plastic) kilichowekwa mdomoni kwa mtoto toka alipozaliwa, kwa lengo la kusukuma oksijen katika mapafu yake.

Mtoto Philippine2

Mtoto Philippine3

Inadaiwa kuwa mtoto huyo alizaliwa na ‘asphyxia’ (tatizo la kutoanza kupumua mara tu baada ya kuzaliwa), hivyo madaktari wamedai kuwa pangekuwa na umeme wangeweza kutumia ‘incubator’ kuokoa maisha yake.

Mtoto Philippine4

Pamoja na jitihada za wazazi hao kutaka kuokoa maisha ya mtoto wao huyo wa kike, mtoto huyo alipoteza maisha siku tatu baadae katika katika hospitali hiyo ya Talcoban.

Mtoto huyo alizaliwa siku tano baada ya kimbunga hicho kuikumba Philippines.

Kutokana na hospitali hiyo kuathiriwa na kimbunga kilichoikumba Philippines wiki iliyopita, wagonjwa wa kituo hicho cha afya wamelazimika kuhamishiwa katika kanisa la hospitali hiyo lililoko ghorofa ya juu ya jengo hilo, ambayo hivi sasa ndio linatumika kama hospitali .

Mtoto Philippine5

Mtoto Philippine6

SOURCE: MAIL ONLINE

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents