Picha: Mrisho Mpoto asherehekea siku ya kuzaliwa na watoto yatima
Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto leo amesherehekea siku yake ya kuzaliwa na kula chakula cha mchana na watoto yatiwa wa kituo cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es Salaam ambapo pia aliahidi kuwasomesha watoto watano.
Mpoto akikabidhi baadhi ya vifaa kwa watoto
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mpoto alisema ameamua kufanya hivyo ili kurudisha fadhila kwa jamii.
“Nimeitwa mara nyingi sana sikuwahi kuja aidha ni kwa sababu ya kuwa na shughuli nyingi lakini pia kupitiwa kibinadamu. Furaha zao walizonikaribisha nazo nimeumia sana. Inaonesha kabisa ni watu ambao walikuwa wanahitaji kuniona,” amesema Mpoto. “Lakini leo nimeona ni siku yangu muhimu ya kuzaliwa na nikaona ni muhimu kusherehekea nanyi siku hii. Tule tufurahi, pia tupeane maneno wawili matatu ili msikate tamaa kwa sababu ya kukosa wazazi. Maisha yetu yapo katika mikono ya Mungu na sisi wenyewe. Pia nimetoa msaada wa vitu vichache kwa watoto hawa pia ninaahidi kuwasomesha watoto watano kutoka kwenye kituo hiki,” aliongeza.
Mpoto akishuka kwenye gari yake
Mrisho Mpoto akiwa na mlezi wa kituo cha Mwandaliwa, Halima Ramadhan
Mrs Mpoto akiwa na watoto
Mtoto akilia kwa uchungu
Mtoto wa Mpoto, Manju akimshikia baba yake mic
Mtoto yatima akilia kwa uchungu baada ya kusikia maneno ya Mpoto
Mzee Chilo akizungumza jambo na watoto
Mrisho Mpoto alijumuika na watoto kwa kula chakula cha mchana
Waandishi,wasanii wa filamu na muziki wakipata chakula kwa pamoja