Burudani

Picha: Mmiliki wa ‘handaki’ la CD za ujanja ujanja Dar atiwa mbaroni na Nape

By  | 

Mmiliki wa hoteli ya Butterfly iliyopo maeneo ya Kariakoo, Phili Ulaya Mdolo maarufu kwa jina la Dotto ametiwa mbaroni kutokana na tuhuma za kumiliki duka kubwa la CD lililopo mafichoni ndani ya hoteli yake hiyo bila kufuata utaratibu wa serikali.


Mmiliki wa hoteli ya Butterfly mwenyeshati la blue bahari akiwa chini ya ulizi wa jeshi la polisi

Dotto amekamatwa Ijumaa hii katika operesheni iliyoongozwa na Waziri Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye ya kukagua maduka yanayouza CD kinyume na sheria pamoja na maeneo yanayozalisha CD feki.

Waziri Nape amesema kuwa huyo ni mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa jijini Dar es Salaam ambao wanafanya biashara hiyo bila kufuata taratibu za serikali huku akiliamuru jeshi la polisi kumshikilia mtuhumiwa huyo kwa ajili ya kutoa maelezo zaidi huku akiahidi kukutana naye siku ya Jumatatu. Tazama picha zaidi hapa chini za tukio hilo.


Waziri Nape akiongoza kukagua baadhi ya vyumba vilivyopo chini ya ardhi katika hoteli ya Butterfly


Kufuli ikivunjwa katika sehemu zilizohifadhiwa CD haramu katika hoteli ya Butterfly


Mizigo ya CD ikiwa stoo katika hoteli ya Butterfly


Muonekano wa moja ya sehemu za kuuzia CD katika hoteli ya Butterfly

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments