Burudani

Picha: Mkubwa na Wanawe yatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima Temeke

Katika kusherehekea kutimiza mwaka mmoja wa Yamoto Band, kituo cha Mkubwa na Wanawe leo kimekabidhi msaada kwenye kituo cha watoto yatima kilichopoa Temeke, Dar es Salaam.

IMG_4727

Akikabidhi msaada huo, mkuu wa kituo hicho, Said Fella alisema: Kabla ya kuzungumza chochote Napenda kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kila jambo ambalo limefanikiwa ni kwa kupitia yeye aliye muweza wa yote.”

IMG_4741

“Pili nawashukuru Watanzania wote karibu kila nyanja kwa kuonyesha ushirikiano wao kwa Mkubwa na Wanawe mpaka kufikia hapa hii leo.Toka ianzishwe Yamoto Band leo ni siku ya furaha kwetu kusheherekea mwaka mmoja ambao umefanyika kuwa na mafaanikio mengi makubwa. Moja kati ya mafanikio hayo ni kuuza kazi zetu kweye mtandao na kukuletea kokote ulipo mpaka majumbani,” alisema.

IMG_4734

Aliongeza: Na kwa hiki kidogo tulichokipata sisi ukijumuisha na furaha tuliyo nayo ya kutimiza mwaka mmoja tumeona ni bora tugawane na wenzetu ambao ni wahitaji haswa kwa msimu huu wa sikukuu kama tulivyozoea kufanya toka kipindi cha nyuma kwani hawa ni sehemu yetu kama wanajamii wenzetu.Na kwa wale wapenzi na mashabiki wa Yamoto Band tupo tayari kukupatia kilicho bora zaidi.

IMG_4743

IMG_4755

IMG_4716

IMG_4727(1)

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents