Picha

Picha: Miss Lake Zone watoa msaada kwa watoto wa mtaani Mwanza

Washindi wa shindano la Miss Lake Zone lililofanyika jijini Mwanza mwishoni mwa mwezi uliopita, wamewatembelea watoto wanaoshi mtaani jijini Mwanza na kutoa misaada mbalimbali.

IMG-20140908-WA0006
Mshindi wa pili wa shindano hilo, Mary Emanuel kutoka Shinyanga akiwapa vyakula na vinywaji watoto wa mtaani jijini Mwanza

Mshindi wa pili wa shindano hilo, Mary Emanuel kutoka Shinyanga, alijumuika na watoto hao kwa chakula na kuongea na wale wenye umri mkubwa na kuwaasa warudi kurudi kwao kuliko kuendelea kuishi katika mazingira hatarishi.

IMG-20140908-WA0001
Mary Emanuel akiongea na watoto hao

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo alikuwa mrembo wa Geita, Rachel Claver na mshindi wa tatu alikuwa ni Nicole Sarakyikya wa Shinyanga.

IMG-20140908-WA0007

IMG-20140908-WA0000

Shughuli hiyo iliandaliwa na waandaji wa shindano hilo, Flora Promotions chini ya taasisi yake ya ‘Nitetee Sauti ya Wanyonge’.

Screenshot_2014-09-03-12-39-47
Washindi wa shindano la Miss Lake Zone lililofanyika Agosti 30 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents