Diamond PlatnumzWema Sepetu

Picha: Mapenzi ya Diamond na Wema Sepetu sio siri tena, wapo karibu zaidi ya kawaida

Diamond Platnumz na Wema Sepetu wameendelea kuliimarisha penzi lao kadri siku zinavyoenda. Uhakika wa kuwa wapenzi hawa wenye uhusiano wa ‘on and off’ wamerudiana kwa kasi, ulijulikana baada ya picha zao wakiwa Hong Kong kusambaa mtandaoni hali iliyopelekea kuzuka mgogoro mkubwa kati ya Diamond na mpenzi wake Penny ambaye kuna tetesi kuwa wameshaachana rasmi.

IMG-20131009-WA0017

Tangu hapo Wema amekuwa haoni aibu kuonesha mapenzi yake kwa Diamond ikiwa ni pamoja na kupromote show ya Diamond ya Christmas.

Kwenye show hiyo ya jana ndipo mambo yalipowekwa wazi zaidi ambapo Wema alikuwa mmoja wa watu waliopanda kwenye stage na kuongea na watoto waliokuwa wakishuhudia show.

379719_654725334570888_100223854_n
Wema akiwa jukwaani kuongea na watoto kwenye show ya Diamond siku ya Christmas

Kwa mujibu wa MillardAyo.com, Diamond alisikika akiuliz: Mnataka kumjua mchumba wangu”? Baadaye wakati akitaka kuimba wimbo wake ‘Ukimwona’, hitmaker huyo aliuliza tena: Naskia ninayetaka kumuimbia wimbo huu yupo humuhumu ndani,” na ndipo Wema Sepetu akapanda kwenye stage wakaimba na kucheza wote.

994992_654719497904805_1370630389_n
Diamond na Wema wakicheza na kuimba pamoja

Katika hatua nyingine baada ya show hiyo, Diamond alichukua private jet na kuelekea Mwanza kwenye show nyingine ya Christmas. Bahati mbaya hakwenda na Wema.

88a9f8ee6d8e11e3aef612ce171e3ceb_8

Picha za show ya Diamond na Milladayo.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents