Burudani

Picha: Mamia wamzika Baba yake Belle 9

Mastaa wa muziki pamoja na wadau mbalimbali wamejitokeza kwa wingi hapo jana, katika mazishi ya baba wa staa wa muziki, Belle 9 aliyefariki akiwa hospitalini mkoani humo usiku wa Machi 18 akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na pikipiki.

Belle akiwa na wasanii pamoja na wadau mbalimbali mbele ya kaburi la marehemu baba yake baada ya mazishi.

Meneja wake, Jahz Zamba, aliiambia Bongo5 kuwa, Mzee Damian amefariki dunia baada ya kugongwa na boda boda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro alikokuwa akiishi.

Alivunja mguu mmoja pale pale na kujeruhiwa vibaya kabla ya kupelekwa hospitali. Dereva wa boda boda naye aliumia vibaya ikiwemo kuvunjika taya na kujeruhiwa kichwa.

Jahz alisema baada ya Mzee Damian kupelekwa hospitali na kuwekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahtuti, kuna dawa zilikuwa zikihitajika lakini zilikosekana kwenye hospitali hiyo.

Ni pengo kubwa kwa Belle 9 kumpoteza baba yake, kwakuwa mara nyingi amekua akidai baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake. Muimbaji huyo anayetokea Morogoro alimtaja mzazi wake huyo kuwa ni mtu anayemuinspire kwa mambo mengi.

Tunampa pole Belle kwa msiba huu mzito na Mungu ailaze roho ya baba yake mahala pema peponi.

Stamina, Afande Selle na wadau wengine.

Mtayarishaji wa muziki, Mona (kushoto) akiwa Morogoro.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents