Tragedy

Picha: Maelfu wajitokeza kwenye mazishi ya Mzee Gurumo kijijini alikozaliwa

Maelfu ya wananchi na watu mbalimbali maarufu wamejitokeza kwenye mazishi ya muimbaji mkongwe wa muziki nchini, Mzee Muhidin Gurumo yanayofanyika katika kijiji cha Masaki wilayani Kisarawe, Pwani.

AMVCA-Trophy-
Muigizaji wa filamu, Jacob Stephen na mwenzake Dude wakisaidia kuubeba mwili wa Mzee Gurumo

Kwa mujibu wa makamu wa rais wa shirikisho la muziki Tanzania, Samwel Brighton, ushiriki kwenye mazishi huo ni mkubwa ambapo mkuu wa wilaya hiyo amewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuweka mambo sawa.

BlQko8uCMAAI4rt.jpg large

“Ushiriki kwa upande wa dansi watu wote walikuwepo kwasababu kama unavyojua huyu ni baba wa muziki huo na wa maigizo tulikuwa nao wengi tu lakini kwa upande wa kizazi kipya kusema ukweli kwa macho yangu sidhani kama nimeona zaidi ya wasanii 10, sijajua tatizo ni nini lakini ushiriki wao ni mdogo kwakweli,” Brighton amekiambia kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio.
1509771_10152345930292558_5133216687622541981_n
Profesa Jay ni miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo

1966668_10152345936327558_2721818766903143162_n
Wananchi wakimzika Mzee Gurumo katika kijiji cha Masaki, Kisarawe

Mzee Gurumo alifariki Jumapili baada ya kulazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Amewahi kuimba na bendi mbalimbali zikiwemo Kilwa Jazz Band, Nuta Jazz Band, Mlimana Park, Safari Sound na baadaye Msondo Ngoma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents